Nenda kwa yaliyomo

Gene Kelly

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Image
Gene Kelly

Eugene Curran Kelly (23 Agosti 1912 – 2 Februari 1996)[1] alikuwa mnenguaji (dancer), muigizaji, mwimbaji, mwongozaji (director), na mbunifu wa mtindo wa kucheza (choreographer) wa Marekani. Alijulikana kwa mtindo wake wa kucheza wenye nguvu nyingi na wa kiatlasia. Kelly alitafuta kubuni mtindo mpya wa uchezaji wa Kimarekani unaoweza kufikiwa na kueleweka na umma kwa ujumla, mtindo ambao aliuita 'uchezaji kwa ajili ya mtu wa kawaida' (dance for the common man).[2][3]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Kelly alizaliwa katika mtaa wa East Liberty huko Pittsburgh. Alikuwa mtoto wa katikati kati ya watoto watano wa James Patrick Joseph Kelly, ambaye alikuwa muuzaji wa gramafoni (phonograph salesman), na mke wake, Harriet Catherine Curran.[4]

Baada ya utafutaji wa kazi usiozaa matunda huko New York, Kelly alirejea Pittsburgh kwenye nafasi yake ya kwanza kama mbunifu wa mtindo wa kucheza (choreographer) katika onyesho la muziki la Charles Gaynor lililoitwa Hold Your Hats kwenye ukumbi wa Pittsburgh Playhouse mnamo Aprili 1938.[5]

  1. ↑ https://www.imdb.com/name/nm0000037/
  2. ↑ https://books.google.co.tz/books?id=meKNAQAAQBAJ&pg=PA71&redir_esc=y#v=onepage&q&f=false
  3. ↑ https://web.archive.org/web/20160221130312/http://www.ranthollywood.com/2014/12/24/best-movie-musicals-of-all-time/
  4. ↑ https://www.britannica.com/biography/Gene-Kelly
  5. ↑ https://www.pbs.org/wnet/americanmasters/gene-kelly-anatomy-of-a-dancer/516/
Image Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gene Kelly kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.